Neno Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2020
Lyrics
VERSE 1
Nimekaa chini Nawaza ni kwanini,
Maandiko yapo lakini itifaki haizingatiwi.
Ukipita msikitini hata kanisani,
ni kama kutinga suti na kiatu bila kiwi.
Watu wanasifu na kuabudu vilivyo,
lakini wengi wao hao ndio waliwamo.
Kelele kelele kuwanyooshea vidole wenzao, kwa makosa makubwa wayatendayo wao.
Nimekuja Gundua tatizo hapa ni Lugha,
ni kama kuzungumza kichaga na Msukuma.
Hawaijui kweli, wanatumia Hisia,
na tena kwa kufwata kanuni za kusukuma.
Ndo mana nimekuja kwenu, Midundo ya Kwenu, tasnia ni ya kwenu lakini Neno la kwetu.
Kufikisha Ujumbe wenu kupitia misingi yetu,
ya kwamba ukiijua Kweli utakuwa Huru.
CHORUS
Napeleka Neno, linapotakiwa kufika
Napeleka Neno, hata pale lilipofika
Napeleka Neno, linakotakiwa kufika
Napeleka Neno, hata kule lilikofika
VERSE 2.
Neno ni nini Neno Neno ni nini?,
Neno ni nini nauliza Neno nini?
Hapo Mwanzo kulikuwako na Neno,
Naye neno alikuwako kwa Mungu.
Naye alikuwa Mungu huyo Neno,
naye Mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Tambua Mwana huru kakuweka huru kweli kweli,
kafungua vifungo na umeijua Kweli.
Yadhuru nini Lakini kwa njia zote ikiwa ni kwa hila au ni kweli neno anahubiriwa.
Kwani neno huyo ndiye mwokozi wa wanadamu mwenye sikio la kusikia na asikie.
Mimi nafurahi, naam mimi Nafurahi,
Mimi nafuraaaaaahi, mimi nafurahi.
Kwani Neno la Bwana ladumu hata milele.
Na neno hilo ni lile jema lililotajwa kwenu.
CHORUS
Napeleka Neno, linapotakiwa kufika
Napeleka Neno, hata pale lilipofika
Napeleka Neno, linakotakiwa kufika
Napeleka Neno, hata kule lilikofika