Imani (feat. Rose Muhando) Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Imani (feat. Rose Muhando) - Jemimah Makau
...
by Phellow 254790511905
*******verse 1********
halelluya
nimwoneeje mashaka
Mungu ninayemwamini
ninayemwamini?
hivi nimwoneeje hofu
Mungu ninayemwabudu
ninayemwabudu mimi?
basi sina mashaka
kwa Mungu nimwabuduye
kwani kwa imani
mambo yote yalifanyika
kwa imani wakati ule
Ibrahimu kamtoa Isaka
tena kwa imani
Sara alipata mimba
nami nitangojea iko siku nitapokea
nami nasubiri siku yangu nitapokea
ah rafiki usinivunje moyo
ah jirani usinivunje moyo
pamoja na kelele nyingi
imani yangu sipotezi
nami namngoja Bwana
yangu itatokea
nami nakaa nasubiri
kwake Bwana nitapokea
*****chorus*******
Basi imani ni hakika
ya mambo yatarajiwayo
ni bayana kwa mambo yale
yasiyoonekana kwa macho
basi nami naamini iko siku nitapokea
(nitapokea nitapokea naaananana)
Basi imani ni hakika (halelluya
ya mambo yatarajiwayo (maaambo)
ni bayana kwa mambo yale (mambo yale)
yasiyoonekana kwa macho
basi nami naamini iko siku nitapokea
********verse2******
basi kwa macho ya nyama
mambo haya hayawezekani
nami namngoja Bwana
Mungu wangu ni kwa imani
yeye atatenda haaa
nitapokea kwa imani
lolote lile niombalo nitalipata kwa imani
YESU ameniahidi
nitapokea kwa imani
basi sivunjiki moyo
iko siku nitapokea
********chorus******
Basi imani ni hakika
ya mambo yatarajiwayo
ni bayana kwa mambo yale (jamani)
yasiyoonekana kwa macho (halelluya)
basi nami naamini iko siku nitapokea
ah nitapokea nitapokea
kwake Bwana eeeeh
Basi imani ni hakika
ya mambo yatarajiwayo
ni bayana kwa mambo yale (yale yote)
yasiyoonekana kwa macho (eheeeeee)
basi nami naamini iko siku nitapokea
*****verse3*****
najua hamnielewi
mambo haya niyanenayo
maana yamefichwa sana
aghalabu mfumbue mafumbo
nami naamini siku moja
nami nitapokea
katika upumbavu wa Mungu
ndipo mema yatatokea
NITAPOKEA IKO SIKU NITAPOKEA
nitasubiri baraka zangu nitapokea
IPO SIKU NITAPOKEA
usinivunje moyo
NITAPOKEA IKO SIKU NITAPOKEA
sikati tamaa
NITAPOKEA
IKO SIKU NITAPOKEA
ahadi yangu kwa Baba
NITAPOKEA
IKO SIKU NITAPOKEA
ninayoyangoja
NITAPOKEA
IKO SIKU NITAPOKEA
JAPO NAONEKANA MJINGA
NINAPOCHEZA NA KUIMBA
LAKINI UJASIRI WA SIMBA
UNAJULIKANA KWA KUWINDA
NAMI NAAMINI SIKU MOJA
MEMA NITAPOKEA
NITAPOKEA IKO SIKU NITAPOKEA
BY PHELLOW 254790511905