BWANA U SEHEMU YANGU MELODIE Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
BWANA U SEHEMU YANGU MELODIE - Sauti Ya Muziki
...
Bwana u sehemu yangu,
Rafiki yangu wewe;
Katika safari yangu
Tatembea na wewe;
Pamoja na wewe,
Pamoja na wewe,
Katika safari yangu
Tatembea na wewe.
2. Mali hapa sikutaka,
Ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka
Sawa sawa na wewe,
Pamoja na wewe,
Pamoja na wewe,
Heri nikute mashaka
Sawasawa na wewe.
3. Niongoze safarini,
Mbele unichukue
Mlangoni kwa Mbinguni
Niingie na wewe
Pamoja na wewe
Pamoja na wewe
Mlangoni Kwa mbinguni
Niingie na wewe.