Alionewa Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2017
Lyrics
Alionewa - Flora Mbasha
...
Alionewa Bwana Yesu,
msalaba Bwana alibebeshwa (× 2)
Alilia Elohi, Elohi Elohi lama sabakitani
Mungu wangu, Mungu wangu,
Mungu wangu mbona umeniacha?
Machozi ya damu yalimtoka Yesu
Kwa uchungu Bwana alisema
Mungu wangu kikombe hiki kiniepuke kama ni mapenzi yako.
Alionewa Bwana Yesu,
msalaba Bwana alibebeshwa
(× 2)
Taji ya miba alivalishwa Yesu
mijeledi Bwana alipigwa.
Alionewa Yesu Alidhihakiwa
lakini Bwana wetu Yesu alivumilia.
Alitukanwa Bwana aliaibishwa
ili mimi na wewe tupate wokovu.
Mungu wangu wasamehe
maana hawajui watendalo.
Mungu wangu wasamehe
maana hawajui lile watendalo.
Alionewa Bwana Yesu,
msalaba Bwana alibebeshwa
(× 2)
Mkuki ubavuni alichomwa Yesu
misumari alipigiliwa.
Kwa sauti Bwana alisema Mungu wangu Mungu wangu ohu wasamehe.
Jililieni ninyi na watoto wenu
Kainamisha kichwa akakata roho.
Jililieni ninyi na watoto wenu
Kainamisha kichwa akakata roho.
Alionewa Bwana Yesu,
msalaba Bwana alibebeshwa
(× 2)
Alionewa Bwana aliteseka Alipigwa Yesu kwa sababu yangu na wewe
Tupate uzima tukombolewe.
Alilia alilia Baba alilia alilia Yesu
Jililieni ninyi na watoto wenu kainamisha kichwa akakata roho.
Jililieni ninyi na watoto wenu kainamisha kichwa akakata roho.
Alionewa Bwana Yesu,
msalaba Bwana alibebeshwa
(× 4)