Yote Tisa ft. Stamina & One Six Lyrics
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2022
Lyrics
Yote Tisa ft. Stamina & One Six - Tommy Thomas
...
Mtaskia mengi, ila yote Tisa
Yeah..
Kichwa mtumba akili spesho
Tommy Thommas
Ringo beats..
Japo nina pumzi, kubomoa kila kitasa, ni maamuzi, *** muhuni naoa sasa
Sina idadi ya midomo nloitembezea kipaza yote tisa Mungu mwema kuwa hapa sikuwaza
Wee mwagizie vyote Roll Royce Japani, utampeleka kote shopping malls Mlimani, mrushe chaka zote waterfalls Miami yote tisa kubwa usimletee utozi chumbani
Mana utabadili njia uache lami ufwate miba, utabadili line usiwe hewani nikipiga, utakimbia mtaani watakudai kwenye msiba yote tisa dawa ya deni kulipa ndo shida
Huna dream huna focus, System inablock us ,unasilim kuwa promoters kwa bia tu unadrop bars,unajiita rap monster, while you can't conquer yote tisa, hii mainstream imejaa maborgus
Ulitaka six pack nikaipata kwa kuhustle, ukaitaka bughatti na sikua hata na ki-passo, nikapewa michapo, Kuna mshua anaishi hapo yote tisa, umaskini kwa mwanaume ni kikwazo
Hustle za mtaa zisifanye, watu ukasujudia we ni wa thamani haijalishi kitu gani unapitia, watakufunga bila hatia, utapingwa na mamia, yote tisa, believe Mungu atafanya njia, Amen.
Amen eyy, mi nasema Amen eyy oh
Amen eyy, linalokuja mbele yangu Amen oh u ohh
Yote tisa, kumi hakuna anaefahamu kesho yake
Yote tisa, kumi ukweli utasimama siku ikifika
Ah, nenda kokote, kuanzia kijiji na tarafa, nini masjidi, na ikibidi ukahiji Makkah Mister pastor,
nenda mpaka Roma kwa Papa, utakufa tu hata uwe roho aba Kama paka
We jifanye body builder upadate mwili wa San Deo, au ikibidi kua modo utokee kila video, tafta pesa wewe ndo kauli mbiu ya leo, bila pesa utaishia tu kuwa baunsa wa mkeo
Yote tisa, kumi waambieni mi sifai, wananita padri mtukutu kwangu bapa ka divai, Biti mkate mgumu namwaga flow kama chai, na hata ningekua ng'ombe haki ya nani ningekua maksai
Huhitaji kuti ili uteleze hembu pambana mwana kwetu, siku hizi hadi wafupi wanamiliki pesa ndefu ndo maisha yetu, wote maskini usilete uchetu, ghetto kuna kunguni kwahiyo chawa usije kwetu
Sio lazima niwe Rasta ili nsambaze mapendo, sio lazima niwe jambazi ili nsambaze magendo, sio lazima niwe msanii ili nsambaze maskendo, ko ukinchukulia simpo usisahau kunchukulia na sendo!
Amen eyy, mi nasema Amen eyy oh
Amen eyy, linalokuja mbele yangu Amen oh u ohh
Yote Tisa, (kumi) hakuna anaefahamu kesho yake
Yote Tisa, (kumi) ukweli utasimama siku ikifika, eeh
Hakuna anayefahamu kesho yake
Ukweli utasimama siku ikifika
Utakula nauli za mkaka wa watu, utazulumu watu, ila yote tisa... Hakuna aliezaliwa kupoteza, ipo siku utailipa na faida pia.
(Ringo beats....)
Added by Renato