Futa Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Futa - PUTTEN ANTHONY
...
nilifundishwa na wazazi wangu,
nishinde ubaya kwa wema,
kulipa kisasi sio fungu langu,
nisije ikosa neema.
ninawaombea adui zangu,
wasio nitakia wema,
sita weka chuki moyoni mwangu,
nitawapenda daima.
je, ulie mwema,
kamwe hautowai matunda mabaya,
machozi yalio matamu,
na machungu hayatoki jicho moja.
tabia ilio njema,
isibadilishwe na watu wabaya,
usiache kutenda mema,
hata kama wanakulipa (mabaya)
sitaki kuzizuia baraka,
kwa kuwaweka watu moyoni,
kurudi nyuma mwenzenu nakata,
nimesamehe niwe na amani,
ooooh isio nitaka,
zitanichelewesha njiani (mimi)
nimetangaza,
saba kwa sabini nimesamehe,
moyo wangu (samehe)
walio kukosea (samehe)
ili uwe na amani,
(samehe usiwaweke moyoni)
moyo wangu,
"uwasamehe," (samehe)
usikubali maumivu (samehe)
uwe na uvumilivu,
(samehe usiwaweke moyoni)
maisha ya dunia,
ni kama,
kupanda na kuvuna,
kile utakacho panda,
ndicho utakacho vuna.
ya nini niyashikilie,
yanayonifanya mimi niumie,
nitanyamaza ili yote yapite,
kwani (ni mambo madogo)
mmmh nita inua macho niangalie,
mtetezi wangu anipiganie,
nitamuita ili anisaidie,
kwani kwake (ni mambo madogo)
maandiko yanasema,
wapende adui zako,
wanaokuudhi waombee,
kisasi si juu yako,
mwachie Mungu,
yeye akupiganie,
usichafue moyo wako,
kwa kuyaweka makwazo yaondoe,
usije naswa kwenye mtego,
katika mawindo yao yakimbie.
mti ulio mwema,
kamwe hautoi matunda mabaya,
machozi yalio matamu,
na machungu hayatoki jicho moja,
tabia iliyo njema,
isibadilishwe na watu wabaya,
usiache kutenda mema,
hata kama wanakulipa mabaya.
sitaki kuzizuia baraka,
kwa kuwaka watu moyoni,
kurudi nyuma mwenzenu nakata,
nimesamehe niwe na amani,
ooooh isio nitaka,
zitanichelewesha njiani mimi,
nimetangaza,
saba kwa sabini nimesamehe.
moyo wangu (samehe)
walio kukosea (samehe)
ili uwe na amani (samehe)
(usiwaweke moyoni)
moyo wangu
"uwasamehe" (samehe)
usikubali maumivu, (samehe)
uwe na uvumilivu, (samehe)
(usiwaweke moyoni)
sasa kubali kufuta (futa)
futa ( futa futa)
maneno yao yote ya hila (futa)
futa (futa futa)
futa usi yakumbuke, (futa)
futa (futa futa)
usiyasumbukie,
moyo wangu (futa)
futa (futa futa)
usije poteza husudi la bwana (futa)
moyo (futa futa)