Umwema Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2018
Lyrics
Umwema - Natasha Lisimo
...
Hee eee! Yeeiyeye wewe ni mwema!
Niliovuka ni mengi
Siwezi tazama nyuma
Kwa visa vingi vitimbwi aii
Ahsante baba
SI kwa akili zangu
wala nguvu zangu mwenyewe
Wewe ni mwema
umenivusha na mengi magumu
Yanayoelezeka na yasioelezeka
Umenifuta maumivu ukanipa Amani
Wa ajabu, fahari yangu, mtetezi wangu
Wewe ni mwema
Mwalimu wangu, shujaa wangu, kiongozi wangu
Wewe ni baba
Ooooooo!
(umenikung'uta mavumbi wewe ni mwema)
Ooooooo!
(umenipandisha pandisha wewe ni baba)
Ooooooo!
(umenifanya chombo cha sifa wewe ni mwema )
Ooooooo!
(umenipandisha pandisha wewe ni mwema)
""
Ungetazama vyeo, uzuri na mali
Mimi ninge kuwa wapi!?
Kiukweli upendo wako hauna kipimo
Umenipenda Bure!
Kwa kupigwa kwako mimi nimepona
Neema yako Kweli ya ajabu
Umenifanya mwanao
Ukanipa uzima na afya
Umenifuta maumivu
Hee ukanipa amani
Wa ajabu, fahari yangu, mtetezi wangu
Wewe ni mwema
Mwalimu wangu, shujaa wangu, kiongozi wangu
Wewe ni baba
Ooooooo!
(umenikung'uta mavumbi wewe ni mwema)
Ooooooo!
(umenipandisha pandisha wewe ni baba)
Ooooooo!
(umenifanya chombo cha sifa wewe ni mwema )
Ooooooo!
(umenipandisha pandisha wewe ni mwema)
Wewe ume kuwa mwanzo
Na bado utabaki kuwa mwisho
Kwenye utata na vikwazo
Bado utabaki suluhisho
Wewe ni taa na mwanga
Humulika popote palipo na giza
Maana hakunaa jambo gumu
Ambalo wewe Bwana unashindwa
Umenipa Amani(Aheee)
Umenipa furaha(Ahee)
Jemadari(Ahee)
Yesu nakupenda
Umenipa uzima (Ahee)
Umenipa heshima (Ahee)
Yesu weee(Ahee) Bwana nakusifu!
Ooooooo!
(umenikung'uta mavumbi wewe ni mwema)
Ooooooo!
(umenipandisha pandisha wewe ni baba)
Ooooooo!
(umenifanya chombo cha sifa wewe ni mwema )
Ooooooo!
(umenipandisha pandisha wewe ni mwema)
Bwana wewe ni mwema
Baba wewe ni mwema