![Barua ft. Daz Nundaz](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/04/05/59f40da34d46488b95b0d85ec47871be_464_464.jpg)
Barua ft. Daz Nundaz Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2024
Lyrics
Barua ft. Daz Nundaz - Dominick DM7
...
oya namna gani mzeee!
aaaah
mbona leo uko hivi ...
aah basi tuh!
vp mchizi wangu mbona naona umesize
unaonekana kama moyoni una majonzi
au dili zako leo haziendi sawa
jinsi unavyoonekana kama umepagawa
niambie ili nielewe
ili na mie nisipagaweeee!
kwangu tangu nimefika nakuona umepooza
ebu niambiee kitu gani unachowazaaa sema basi ni nn kinachokusumbuaa nafsi
niambiee basi au kuna kitu kimekugasiii
Aaaah! we boraa acha tu wangu mkachaaa
ni stori ndefu nikianza kukupa
ubongo wangu nahisi kama unaweza athirika kwa haya matatizo makubwa yaliyonifika
shemeji yako nadhani unamjuaa ambaye kichwa changu alikichemvuaa
baada ya kuishi mda mrefu na wangu laziziii!
nikabidi niende kuwaatarifu wazazi kwamba nishampata ambae ntafunga nae pinguu za maisha
na nilikuwa nauhakika hakuna ambae atatutenganishaa
basi bhna baada ya kurudi yangu safari nikakutaa mlango wa Geto umepigwa kufuli
Nauliza watu wote sipati Jibu Ni mkasa mkubwa mwenzako ulionisibu
nikaanza kulisaka Tunda langu kwa sana , lakin jitihada mwisho zikashindikana
nikaamua basi tuh ni kutulizana
nikawa sitoki nje niko ndani tuh nalala , huku mawazo mengi kichwani yamenitawala
Chorus
katika mahaba tulishazama kimwili
lakin barua niliyopokea
nashindwa hata kuamini
ua la moyo wangu halipo tena na mm
barua hii jaman inanihuzunishaa
ninasoma kwa moyo wangu inasoneneka
na ufukara ndio umetutenganisha
subiri basi stori nikumalizie, eeeenhee
mkasa huu mwanangu ulionifika miee , eeeenhe
hususa ni kama baada ya wiki kadhaaa
ndipo hapo nikapokea baruaaaaa
kilichokuwa ndani sikuitambuaaa
nikaja kuielewaa baada ya kuifunguaaa
nikakutaa barua yenye ujumbe mzito
ikiwa imeambatana na kadi ya mwaliko
ndege ameluka hayupo tena nami
sasa ivi sijui mwenzangu mm nani
hali yangu duni imefanya kuelemewa
na hivi karibuni demu wangu anaoelewa
barua inanisisitiza harusini nihudhurie
sijui hata siku io hata wapi mi nianziee
Mpenzi umeniacha kwenye Nyavu nimenasa
nimebaki kama kipofu , sioni pa kupapasa
nikisoma barua, kumaliza huwa nashindwa
kwani nahisi kama unatonesha donda
shika mwenye usomeee baruaa hiii!
Soma mwenyew uone baruaa hiii! ×2
Ikufikiee wangu wa enzi mpenzi
mi kiafya mzima natuamaii nawe kiafya uhaiii
dhumuni la barua ni kukutaka nawe kujua
Nini ni hasa , na ni kipi kisa na mkasa kilichonishawishi
mbali nawe kwenda kuishi, sio siri mm binafsi sikupenda kuishi maisha ya duni ya chini sana kumbuka ufukara ,
umasikini kututengaaa vimechangiaa ilo usipingee bahna sasa nani alaumiwe unadhani hivi punde me natarajii
kufunga pingu maishani ili niishi maisha ya thamani yaliyo ya gharama tena adimu kama almasi fanya Jina usikose harusini ukipata nafasi kwenye barua hii nimeambatanisha kadi hii ya mwaliko yako
basii usimalizieee kusomaaaa
basiiiiiiii usimaliziee kusomaaaa
kwan ukiendeleaa moyo wangu unauchoma
kwa kuondoka wangu huyu mpenzi
moyo wangu umejawa na simanzi
niliamini tutatenganishwa na umauti
sasa amekubali fukara hana sauti
Mola ndie anaegawa umasikini na Utajiri
nae hali yake binti ameshindwa kuhimili
ndo maana leo unaniona nimeshikaa tamaa
ni sawa na kifaranga aliekosa mama
aliyemjali aliyemjali ndie aliyenipa mm ufukara
lakini naamini ipo siku nyota yangu itang'ara
Chorus
katika mahaba tulishazama kimwili
lakin barua niliyopokea
nashindwa hata kuamini
ua la moyo wangu halipo tena na mm
barua hii jaman inanihuzunishaa
ninasoma kwa moyo wangu inasoneneka
na ufukara ndio umetutenganisha ×2