Mshindi (Remix) ft. Stamina Shorwebwenzi Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2023
Lyrics
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona
Eh
Tushaokota sana Vyuma chakavu hadi makopo
Magari ya makoa Saivi tupo na mikoko
Saivi big name big fame Yani kila chocho
Hadi kondeboy hangoji hela ya korosho
Sisi ndio wale mtaani waliamini hatuwi mabingwa
Walituzimia data kisa simu za vizinga
Nyumba za tofali hazina rangi wala skimming
Toka kuoga bwawani mpaka leo kwenye Swimming
Si ndio wale skonga tulipass tu kwa chabo
Walio tuzidi akili wengi wao mambo bado
Tuliosha sana vyombo na wakatutupia vilago
Hata uumwe gonjwa gani dawa ilikua panado
Mlitukata miguu Mungu akatupa mwendo
Mlitutegea miba Mungu akatuvisha sendo
Mlitupa mifupa na sisi tunamapengo
Leo mipango imenyooka iliyopinda kila angle
Tumelelewa na mitaa tuna ndugu
Nashida zimetufanya tue masugu
Tushatembea sana kwa miguu
Sasa ni zamu yetu kua juu
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona,
Waona nini ukiniona
watizama mshindi
Tushazika wazazi
Dunia ikawa ndo mlezi
Tukateswa na maisha
Yani hakuna mtetezi
Kwetu sukuma wiki
Ili sukuma mwezi
Na mapambano ya dhiki
Tuka muachia mwenyezi
From zero to hero
Nobody to somebody yeah
No mummy no daddy
But am struggling
Maisha yanavuruga
Shida za kila muda
Mpaka marafiki
Wakageuka yuda
Tumelelewa na mitaa tuna ndugu
Nashida zimetufanya tue masugu
Tushatembea sana kwa miguu
Sasa ni zamu yetu kua juu
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona
Waona nini ukiniona
Watizama mshindi ukiniona,
Watizama mshindi