MFALME ft. INKMAN BC Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2023
Lyrics
Ayeee
iNkmaN
Heri nusu shari kuliko shari kamili
Masalkheri, aheri
Utamu wa mziki, bendi
Maskini ni maskini tuu, hata katiba wakiamendi
Mwanzo, kujiunga kidato ilikua balaa
Si hela, si alama
Nashuku irizi na ganga ganga za hao niitao familia, shuksha
Lakini bado shukran, niliweza kujipigania
Saa hii niko kwenye usukan
Maisha hukuwa ni subra
Msikize sultan, labda atakueleza kusiko dhiki abadaan kataan
Ayee
Ushairi ni utanashati wa muundo wala si mwandiko
Bighairi ya bangi, me huvuta pumzi tuu
Ushuzi si harufi bali hewa tuu
Utunzi ndio baraka
Mbaraka ni mtunzi
Maneno sadaka tuu
Mahindi na mtama zote nafaka tuu, lakini tui yenye fanaka ndio maziwa na vice versa
Mchuzi tutaunywa iwe ni dagaa au papa, tofauti idadi ya vitunguu labda
Moshi si moshi ka si ya shada
Pochi la biashara ni rizla ndani, bandana, Balloon Clan family, purple ndo colour
Flavour ni mbichwa tuu, favours doo
Love hearts niko cardi boo
iNkmaN daktari
Marrapper ni sugu kama ugonjwa hatari lakini darasani wataketi, madaftari wataseti
Hati ni moja tuu, wino na harufu ya damu
Hao Corona mafua, me bado virusi vya ukedi utadedi mwanangu
Na si siri,
Mchele si staftahi,
Ata kaburini msinifunge tai
Ayee
Chuo kikuu kilinifanya niwaone wahenga waongo
Ati baada ya dhiki, faraja, sukuma baada ya sukuma, wiki imefika Ijumaa
Upende usipende, chooni utachuchumaa...
Utungo nlianza nikiwa tumboni sistuke mbona iNkmaN kakomaa
Nadra sana kupata zabibu kwenye kapu la tufaha
Malenga akinena, sogora na gonga gonga zake bado kwa kijiji ni mzaha
Utamu wa pombe ni marafiki na furaha
Twende bar basi
Rhyme after rhyme, tamu ka na-na-si
Tangu ukoloni ,kiberiti bado kifaru na fa-ra-si
Mgema akisifiwa chunguza sticker labda unakunywa ma-ka-ma-si
Bado swali nauliza, wapi mfalme?
Nani mfalme?
Simaanishi kutangaza vita lakini naangazia tuu, wapi mfalme?
Zimepita miaka, zimebadilika karne, tumefika kenda, tulipita nane
Tumezua zogo, mawe kwa afande
Elfu noti ndio kipande
Labda korti lakini utalala rumande
Kwetu jangwani, tunaoga kwa umande
Peace, nasimaanishi supu wala kamande.
iNkmaN BC, the biggest Balloon.