Malkia Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2022
Lyrics
Malkia - Benkai Music
...
Benkai oh yeah
ooh ooh (Double A)
Maneno mengi nimesema kwako
ya kupagawa
Madhila mengi nimetenda kwako ooh
Ila sio sawa
Na ulijitolea nitunzia maisha sina cha kukulipa eeh iyeah
Na pamoja na visa kwa kuudhi kabisa mbali hukunitosa aah
Kile kidogo cha kuokota
Ndio pia unanilisha
Na lako tumbo lasokota
Bora mimi nimepata
Kesho asubui unajikokota
Ili uzidi kutafuta
Mimi ni dua kukwombea Mola
Uchungu wa mwana, aujuaye mzazi
Sitakudharau mama, nisije pata maradhi
Mimi bado kijana, sijamudu na kazi
Ipo siku ntachanua, ntakuonea radhi
Nakwita nakuita malkia
Na Mola akubariki pia aaah
Akupunguzie mashida (shida)
Akuongezee baraka
Akuondolee mashaka (mashaka)
Akuongezee na miaka haaya
Nikikulaghai na kukupiga chenga
Na pia kukudharau
Najua sifai ila bado wanipenda
Huwezi kunisahau
Na upendo wako sio kama wa mabinti
Wa kutaka visenti
Na fadhila zako kwangu kamwe hazifichiki
Nakupenda kishenzi
Na moyoni mwako wafadhili kama benki
Hizo hisia za mapenzi
Mimi mwana wako unafiki mi siweki
Kwangu mimi we riziki
Uchungu wa mwana, aujuaye mzazi
Sitakudharau mama, nisije pata maradhi
Mimi bado kijana, sijamudu na kazi
Ipo siku ntachanua, ntakuonea radhi
Nakwita nakuita malkia
Na mola akubariki pia aaah
Akupunguzie mashida (shida)
Akuongezee baraka
Akuondolee mashaka (mashaka)
Akuongezee na miaka haaya
Hakuna oh hakuna ah, wa kukureplace
Namshukuru Maulana
Kwa kunibariki, kuwa na wewe
uuuuuuuuuhhh
(Kaiboy)
Nakwita nakuita malkia
Na Mola akubariki pia
Akupunguzie mashida (shida)
Akuongezee baraka (baraka)
Akuondolee mashaka (mashaka mami)
Akuongezee na miaka haaya