Maneno Ungakusanya Lyrics
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2014
Lyrics
Maneno Ungakusanya - Maulidi Juma
...
Ewe bingwa wa mabingwa bingwa uso na kifani*2
ulisema nimetengwa nami nikawa makini
kuwaje leo warengwa hunitoi midomoni*2
CHORUS
Maneno ungakusanya wapitao ukawapa basii hungenisengenya ni kwamba waniogopa*2
ungetuonya ni yapi ambayo umeyafanya
uno ni mwaka wa ngapi pia sote twabambanya
na kiwa huniogopi ya nini kunisengenya
Siku zote nakwambia asubuhi na jioni*2
Mungu ni wa sote pia ondosha wivu moyoni*2
Wewe usiesikiia huvuna mnagani*2
Mimi sikukasirika nafanya kama utani*2
kumbe wewe wakereka kuwemo nami kundini*2
Nkawa na kutheka hunalo langu la ndani*2
Maneno hili na hili moyo wangu wauvunja
Lolote lingatuwili mwenda zake lenye kuja
hakna mungu wawili bali Mungu ni mmoja*2
kiwa una mungu wako asiekuwa wetu sote
mpe zile tahaliko ili uje unisute
kielewe cheo chako kitadumu siku zote*2