Penzi Sirini Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2022
Lyrics
Verse 1:
Mh, mmmhmmm mmmmmh….
Mara keshooo oh, ni penzi gani la magendo,
Naomba ukweli unambieeee,
Ni vicheshoo oh, washikaji zako wanataka mpaka kuwa na mie,
Penzi sirini sirini, mie nakonda huku wewe unanilisha yamini,
Eti liwe la chini kwa chiniii.. unanipatia shaka kukuamini…
Bridge
Kama kuna mwengine mie uniteme, kidogo dogo jua lizame,
Akili ihame, moyo upambane kuliko kuumiza roho
Chorus
Liwe wazi sasa, liwe wazi sasaaa
Liwe wazi sasa, kama sio leo basi isiwe kesho
Liwe wazi sasa, liwe wazi sasaaa
Liwe wazi sasa, kama sio leo basi isiwe kesho
Verse 2:
Uuhuuu uh uuuhuuu..
Natamani natamaniii… ila haiwezekani
Huba limezidi kisirani, nahitaji la Fulani aaah…
Kwa dhati nalia, sijaridhia ah,
Hii hali naona unahifurahiaa..
unanipenda kweli ama unanitania
Nawaza peke yangu usiku naliaaa…
Iwe mtaani mahug kiss kidogo,
Nikuite honey, madeko yenye mikogo,
Wa kibarazani, tusiyajali tuwape visogooo
Basi kubali, mpenzi tumalize zogooo