Boom Focus | Tunamuangazia Dulla Makabila
Wapo wasanii wengi wa Singeli nchini Tanzania lakini Dulla Makabila ni msanii halisi wa Singeli.
Ni miongoni mwa wasanii wa Singeli ambao wamekuwa wakifanya vizuri sana tangu alivyoanza kufahamika pale alipoanza kuimba.
Kazi zake murua kuanzia Hujaulamba, Utatoa Hutoi na hata ule uliozaa jina la Makabila ni moja ya kazi zilizomtangaza sana mwimbaji huyo.
Kila ngoma ambayo ambayo Dulla Makabila amekuwa akiachia ni jiwe na mashabiki wamekuwa wakipokea kwa uzito mkubwa.
Ngoma ambazo amefanikiwa kuachia mpaka sasa ni 'Jambo La Kheri', 'Gari Langu', 'Naacha Muziki', 'Wakunizika', 'Nikizipata', 'Nitakuwaje', 'Mnyama', 'Waongo', 'Nimeghairi Kufa', 'Sema Kweli', 'Nikizipata' na nyinginezo.
Kwa sasa anatamba na ngoma mpya ambayo imekuwa habari ya mjini 'Pita Huku'. Ni bonge moja la ngoma ambapo anazungumzia uhalisia wa maisha katika jamii tunazoishi.
Anazungumzia namna gani wale ambao wanafanya mambo kinyume na matamanio ya Mungu watapata hukumu yao siku ya mwisho wa dunia.
Anazungumzia walevi, mashoga, wezi, malaya na watu wote wanaotenda mambo kinyume ya maadili ya maaamrisho ya Mungu kwa jumla jinsi watakavypata hukumu yao.
Hakika ni wimbo mzuri sana kuusikiliza na zaidi kuutazama kwenye video yake ambayo imetengenezwa kwa ustadi mkubwa. Huyu ndiyo Dulla Makabila ambaye watu wamekuwa wakimfahamu kwa muda mrefu sana.
Endelea kusikiliza ngoma yake ya 'Pita Huku' hapo chini kupitia Boomplay!
#BuzzBrandColumn #BoomFocus #Music #DullaMakabila #Trending
Comments (27)
New Comments(27)
Broooh Qubic
franciscu7qx
imeisha iyoo
mrsinia
Kazi nzur sana mung azidi kumbarik kila kukicha awe ni wakutoa hit song zilizoenda shule kama hizi
inocentd9c1i
wapumbv pit kule
146492345
na wakinga wotee pita hukuuu
Jeremiah 26 life
wemsukuma pitauku
cute vanilla
hgra san bro
Dabob bbbbb
Welcome to Gboard clipboard, any text you copy will be saved here.
Adam Mambala
1000
Benard Kyasi6kg61
weee muhaya pita huku
mosha ze95p
moto sanaaa
Rashid Mashaka
Yani
kazi Nzur broooh hkuna tbu