Boom Top | Ngoma kumi kati ya 100 zilizotamba Boomplay wiki hii hizi hapa
Leo ni Jumatatu murua, siku ambayo tunamulika ngoma ambazo zimefanya vizuri ndani ya orodha ya ngoma 100 wiki iliyopita.
Katika kuhakikisha hili linakwenda vizuri, tunakusogezea ngoma 10 ambazo zimeongoza kwenye chati wiki iliyopita.
1. Puuh ft Jay Melody - Billnass
Hii ni ngoma kali kutoka kwa Billnass akimshirikisha moja ya wasanii ambao wamefanya vizuri sana mwaka huu kwenye app ya Boomplay, Jay Melody. Puuh ni ngoma ambayo inajidhihirisha namna ladha mbili kutoka HipHop na Bongo Fleva zikichanyika zinatoa muziki mzuri sana. Pengine hii ni ngoma ya kufungia mwaka kutoka kwa Billnass.
2. Nitongoze ft. Diamond Platnumz - Rayvanny
Ni ngoma kutoka kwa staa wa muziki Tanzania, Rayvanny 'Nitongoze'. Ngoma hii mpaka sasa imeendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kukaa nafasi ya pili baada ya kudumu nafasi ya kwanza kwa wiki kadhaa katika orodha ya ngoma 100 bora Boomplay.
Nitongoze ft. Diamond Platnumz
3. Yataniua ft. Diamond Platnumz - Mbosso
Yataniua ni ngoma ambayo inapatikana kwenye EP mpya ya Mbosso inayojulikana kwa jina la Khan. Ngoma hii yenye mahadhi ya Amapiano ni kali sana na amemshirikisha Diamond Platnumz. Endelea kusikiliza ngoma hii hapo chini.
4. Lonely ft. Abbah - Marioo
Loney ni ngoma kali kutoka kwenye albamu ya Marioo 'The Kid You Know'. Ni ngoma ya tatu kutoka kwenye albamu akiwa amemshirikisha Abbah. Endelea kusikiliza ngoma hii hapo chini kupitia Boomplay.
5. Kwikwi - Zuchu
Ngoma hii kutoka kwa Zuchu Kwikwi ni ya Mapenzi ambayo Zuchu anaonesha ni kwa kiasi gani anampenda mpenzi wake huku akimsihi mpenzi wake huyo asimuache kwani anaogopa kuumbuka na kupata aibu mbele za watu.
6. Huyu Hapa
'Huyu Hapa' pia ni ngoma kutoka kwa Mbosso inayopatikana kwenye EP yake ya 'Khan'. Ni ngoma ya kwanza kabisa kwenye EP na ina ladha fulani ya miondoko ya mduara. Inapendeza sana kupigwa kwenye sherehe hususani harusi.
7. Nidhibiti ft. Zuchu - Jux
Huu ni wimbo kutoka kwenye albamu ya Jux 'King Of Hearts'. Ni ngoma kali ambayo imepambwa kwa ustadi wa juu na uwepo wa msanii mahiri wa muziki Tanzania, Zuchu.
8. Shetani ft. Costa Titch & Alfa Kat
Ngoma hii ya Amapiano kutoka kwa Mbosso akiwashirikisha Costa Titch & Alfa Kat inapatikana kwenye albamu yake ya 'Khan'. Ni bonge moja la ngoma ambayo haichoshi kusikiliza muda wote.
Shetani ft. Costa Titch & Alfa Kat
9. Cough (Odo) ft. Empire - Kizz Daniel
Baada ya kutamba muda mrefu na ngoma yake Buga (Lo Lo Lo), ngoma nyingine ya Kizz Daniel 'Cough (Odo)' imeanza kutamba kwa kuingia kumi kumi bora ya 100 bora ndani ya app ya Boomplay.
10. Champion ft. Nay Wa Mitego - Kontawa
Ngoma hii kali kutoka kwa Kontawa ni kali na inazidi kudhihirisha ubora wake kadri siku zinavyozidi kwenda. 'Champion' ni ngoma fulani ya kutia moyo inayoelezea mapambano ya maisha. Uwepo wa Nay Wa Mitego umezidi kuongeza chachu ya wimbo huu kuwa bora zaidi. Sikiliza ngoma hii hapo chini.
Wimbo gani umekuvutia kwenye orodha hii?
#BuzzBrandColumn #BoomTop #Music #Trending
Comments (23)
New Comments(23)
130395011
Lucyf0xi7
Zote ni
Young mapishi
Fantastic
metusela imani
wtf
Emanuel Edwardgnfrf
nc
Regina Joel kabalibalit03i6
zuchu ni mzuri kuliko nandy[0x1f641]
officially ree
khan mbosso❤️❤️
denis fauatine
all are my best songs
deekson360
nitongoze by vee van boe"chuiiii"[0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f]
Priphan
Puu
puu na nithibiti jamani