Loading...

Download

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

2022 umekuwa mwaka mzuri kwa tasnia ya muziki wa Tanzania, tukishuhudia kuibuka kwa wasanii mbalimbali wanaochipukia, wasanii wakijituma zaidi ya kawaida kwenda kwenye viwango vyajuu na kutambulika kimataifa. Mwaka 2022 umeshuhudia wasanii takriban sita waTanzania wakijiunga na ‘Boomplay Golden club’. Hii ni klabu mahususi kwa wasanii waliopata wasikilizaji zaidi ya milioni mia moja Boomplay huku Tanzania ikiwa nchi ya pili kwa kuwa na wasanii wengi baada ya Nigeria.


Katika kufunga mwaka huu mzuri katika tasnia ya muziki, App namba moja kwenye utoaji wa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, Boomplay, imetoa takwimu zake za kila mwaka ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu.


#BoomplayRecap2022 hutoa muhtasari wamatumizi ya muziki na uchambuzi kuhusu ladha na machaguo ya wasikilizaji ndaniya mwaka. Pia, huwawezesha watumiaji wa App kupata orodha zao binafsi za nyimbobora, wasanii, albamu na aina ya muziki.


Boomplay Recap inawasilisha data na uchambuzi kuhusu matumizi ya muziki Boomplay huku ukaguzi ukifanyika katikakipindi mahususi. Inaangazia na kugawanya data za muziki kulingana na nchihusika, wasanii na watumiaji na kwa kufanya hivyo, hutoa taswira halisi yausikilizaji wa muziki na tabia za kujihusisha na muziki kwa tasnia za ndani baraniAfrika.


Usahihi na umuhimu wa data na chati za Boomplay kama picha sahihi ya matumizi ya muziki inategemea msingi wa watumiaji wa Boomplay, ambao kwa kiasi kikubwa ni demografia ya tabaka la chini na la kati ambayo ni sehemu kubwa zaidi ya watu katika bara.Hivyo ni jumuishi na hunasa ladha ya muziki wa ndani na tabia za watumiaji wamuziki.


Usikilizaji wa muziki Boomplay umekua kwa mwaka wa 2022 kwa asilimia248, ukichangiwa na watumiaji wake milioni 88 wanaotumia App kila mwezi naongezeko la idadi ya nyimbo Boomplay zaidi ya milioni 90.


Kwa mwaka wa 2022, Boomplay Recap kwa kila nchi inaangazia kategoria mbalimbali kama vile;- Wasanii Bora waKiume, Wasanii Bora wa Kike, Wasanii Wanaovuma Zaidi, Nyimbo na Albamu Zilizosikilizwa Zaidi, na nyinginezo, huku Recap ya wasanii ikitoa takwimu za mwaka 2022 za wasanii binafsi, ikiwa ni pamoja na usikilizwaji wa jumla, masaa ya usikilizwaji, Wimbo Uliosikilizwa Zaidi na Nchi ambayo msanii Amesikilizwa Zaidi.


Kwa upande mwingine, watumiaji wa App ya Boomplay (Boombuddies) watapata taarifa binafsi kuhusu matumizi yao ya muziki naushiriki wao kwenye App ya Boomplay kupitia ‘Users Recap’ ambayo inaangazia safari yao ya muziki kwa mwaka 2022 kwa kutoa maelezo kama vile idadi ya nyimbo walizosikiliza, aina ya mziki wao pendwa, muziki mpya, wasanii maarufu, nyimbo walizozirudia mara kwa mara na taarifa nyingine binafsi za kuvutia.


Kulingana na taarifa kutoka kwenye Boomplay Recap Tanzania, Diamond Platnumz, Harmonize na Marioo ndio wasanii watatu wa kiume walioongoza kusikilizwa zaidi kwenye kipengele cha ‘Wasanii Wa Kiume Waliosikilizwa zaidi’ huku kwa upande wa wasanii wa kike, Zuchu, Nandy na Maua Sama wakiwa kwenye kipengele cha ‘Wasanii wa kike Waliosikilizwa Zaidi’. Ni vyema kutambua kuwa Zuchu amekuwa akiongoza kipengele hiki kwa muda wa miaka mitatu mfululizo sasa.


Katika kipengele cha Wimbo Uliosikilizwa zaidi Boomplay kwa mwaka 2022 ni wimbo wa Jay Melody ‘Nakupenda’. Wimbo wa Marioo ‘Naogopa’ aliomshirikisha Harmonize ukikamata nafasi ya pili, huku ‘Utu’ wa msanii Alikiba ukikamata nafasi ya tatu.


Komando Wa Yesu anaongoza katika kipengele cha nyimbo za Injili kupitia wimbo wake uliopata umaarufu mkubwa unaofahamika kama ‘Yamebadilika’ ‘Neema Semfukwe anashika nafasi ya pili na wimbo wake unaofahamika kama ‘Ndio’, huku 'Ni Wewe' wa Mathias Walichupa ukinyakua nafasi ya tatu. 'Ni Wewe' ni wimbo ulioingia kwenye kipengele hiki kwa mara yapili mfululizo sasa.


Wasanii wa Tanzania Walioshamiri Zaidi kwa mwaka 2022 ambao wamekuwa na mwaka mzuri wa ukuaji ni pamoja na;- Jay Melody, Marioo na Phina kwa kila mmoja kuwa na wimbo ambao umepata wasikilizaji zaidi ya milioni 10. ‘Nakupenda’ ya Jay Melody ikiwa na wasikilizaji zaidi yamilioni 44.5, Mi Amor ya Marioo ikiwa na wasikilizaji zaidi ya milioni 32.7 na Phina ‘Upo Nyonyo’ ikiwa na wasikilizaji zaidi ya milioni 10.8M.


Baadhi ya mambo mengine kulingana na data za wasikilizaji wa Tanzania kwa 2022, ni pamoja na Wimbo Uliopendwa na Watanzania Siku ya Kwanza ya Mwaka 2022 ambao ni wimbo wa Diamond Platnumz ‘Unachezaje’. Katika Siku ya Wapendanao ya mwaka 2022, Wimbo wa ‘Mwambieni’ wa Zuchu ndio wimbo uliosikilizwa zaidi. Wimbo unaopendwa kusikilizwa nyakati za asubuhi ni wimbo wa Christina Shusho ‘Shusha Nyavu’ na Wimbo Unaopendwa Zaidi Usiku Wa Manane Kwa Mwaka 2022 ni wimbo wa Marioo Mi Amor wenye maHadhi ya acoustic.


Boomplay imekuwa mstari wa mbele katika mapinduzi ya usikilizaji wa muziki barani Afrika. Imedhamiria kutumia ushirikiano wa kimkakati na mipango ya maendeleo ili kuwezesha mfumo wa muziki kidijitali wa Afrika kutambua uwezo wake. Ushirikiano wa hivi karibuni na Redioya Generations ya nchini Ufaransa na Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO Tanzania ni hatua ya kukuza maendeleo ya utamaduni wa usikilizaji muziki kidijitali na utumiaji wa muziki kwa njia ya halali huku ukipanua wigo wa wasanii kimataifana kusaidia tasnia ya muziki wa Tanzania kuwa na manufaa zaidi na yenye manufaa kwa pande zote.


Playlists za#BoomplayRecapTZ2022 kwa sasa zinapatikana kwenye App ya Boomplay kwenye mahadhi ya aina tofauti ya muziki, zikijumuisha wasanii wote na nyimbo zao na zaidi ili watumiaji wafurahie na kuhuisha nyimbo na matukio wanayopenda ya 2022. Playlists hizo zinapatikana kwenye sehemu ya ndani ya App ambayo imepewa kichwa cha ‘Boomplay Recap 2022’.


Wasanii Wa Kiume Walioongoza2022

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

1. Diamond Platnumz

2. Harmonize

3. Marioo


Wasanii Wa Kike Walioongoza 2022

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

1. Zuchu

2. Nandy

3. Maua Sama


Nyimbo Zilizoongoza Kusikilizwa2022

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

1. Nakupenda-Jay Melody

2. Naogopa-Marioo ft Harmonize

3. Utu-Alikiba


Wasanii Walioshamiri 2022

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

1. Jay Melody

2. Marioo

3. Phina


Albamu Zilizoongozwa Kusikilizwa2022

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

1. First of All-Diamond Platnumz

2. Love Sounds Different-Barnaba

3. Only One King-Alikiba


Nyimbo Zilizoongoza Kwenye Chati

Diamond Platnumz, Zuchu, Harmonize, Nandy vinara Boomplay 2022

1. Naogopa-Marioo ft Harmonize

2. Nakupenda-Jay Melody

3. Utu-Alikiba


Itazame Orodha kamili hapa:-

https://Boom.lnk.to/BoomplayRecapTZ2022

Comments (46)

0/500

    New Comments46

    mrsinia

    hapo kwa jeshi mmeyumba kidogo alistahili kukaa no.1 maana amekuwa ni hit maker takriban mwaka mzima na kwa upande wa female artist namba 2 . alistahili Nandy maana zuchu anabebwa na label tu no new pale

    Tanzania

    jemesimuheree@gmail.cotkb4d

    mwita

    Image | Boomplay Music
    Tanzania

    piuskkaxl

    diamond

    Tanzania

    shiza39049

    Bad nation

    Tanzania

    addie mg

    platnumz

    Tanzania

    Sam Edward zidkp

    harmonize hatari. vp chui kapotelea msituni au vipi

    Tanzania

    yuzzotz956

    daah kweli imebidi wapate pongezi

    Tanzania

    Icah Mecky

    By my name is ICAH MECKY

    Image | Boomplay Music
    Tanzania

    illuminati brotherhood wci24

    GREETINGS… how you interested of joining the illuminati brotherhood society call number +2348142081555 so you can become A full member of the illuminati brotherhood society, you have been invited to join the illuminati organization and become? *RICH *FAMOUS *POWERFUL *PROTECTED Remember a welcome package of 2.5 million naira to your account details frist BY the great illuminati organization and after your initiation you will recieve your second benefit which is ten point five millions us dollars and more to benefit ($10.500,000) if interested Nigeria inbox us on whatsapp or call +2348142081555

    Nigeria

    liki0avt3

    diamond

    Tanzania

    +

        -   or   -

        -   or   -

        NG +234

            Please Select A Playlist

            Add New Playlist

            Share on

            Embed: Love & Light EP

            Custom Size :

            • Default
            • Desktop(300*600)
            • Mobile(300*250)

            Type :

            • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
            Get Boomplay Premium
            for
            Payment Method
            Pay With
              Review and pay
              Order Date
              Payment Method
              Due Today
              Flutterwave
                Subscription Successful

                Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

                Now you have access to all the features of Boomplay App.
                Payment Failed

                Please check your balance and then try again.

                You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
                Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
                Payment Processing...
                10 s

                Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

                Payment Processing
                Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
                About Order Status