Loading...

Download

Boom Focus | Tunamzungumzia Nedy Music

Nedy Music ni miongoni mwa wasanii mahiri wanaosifika kwa nyimbo za mapenzi.


Jina lake kamili, Said Seif Ally na asili yake ni Zanzibar. Anasifika kwa kuimba nyimbo za Afropop, Zouk na Bongo Flava.


Kabla ya kuwa msanii, alikuwa mahiri sana kwenye kucheza yaani dansa, na alitumbuiza kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki kwaajili ya kukuza kipaji chake.


Mwaka 2010 akiwa pamoja na kundi lake, alishiriki kwenye shindano la Dance La Fiesta na kuibuka washindi wa shindano hilo. Mwaka 2011, alishiriki katika shindano la 'Dance Mia Mia' lakini isivyo bahati akashindwa kufika fainali.

Boom Focus | Tunamzungumzia Nedy Music

Kipaji alichonacho Nedy Music kimetengenezwa kuna kituo mahiri cha kukuza na kulelea vipaji vya muziki maarufu kama Tanzania House Of Talents (THT), ambapo alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na kufanikiwa kuhitimu.


Katika kujitafuta kwake kimuziki, Nedy amewahi kufanya kazi chini ya Ommy Dimpoz kupitia lebo ya PKP Entertainment Music Label na kufanikiwa kuachia wimbo wa 'Usiende Mbali' ambao alimshirikisha Ommy Dimpoz na kumfanya taratibu kuanza kutambulika kwenye tasnia ya muziki.


Baada ya hapo rasmi tasnia ikaanza kumtambua na ndipo alipokuja na ngoma yake ya 'Rudi' aliyoiachia mwaka 2016 akimshirikisha mzee wa masauti Christian Bella.

Boom Focus | Tunamzungumzia Nedy Music

Mpaka sasa, ameshafanikiwa kuachia nyimbo zaidi ya thelathini ambazo zinapatikana rasmi kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki. Miongoni mwa ngoma hizo ni 'Usiende Mbali', 'Rudi', 'Dozee', 'Nishalewa', 'One And Only', 'Homa La Jiji', 'Zungusha', 'Mi Nawe', 'Carino' na nyingine nyingi.


Kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya 'Simpi Talaka' ambayo inapatikana Boomplay. Endelea kusikiliza 'Simpi Talaka' hapo chini.

Simpi Talaka

#BuzzBrandColumn #BoomFocus #Music #Trending #NedyMusic

Comments (11)

0/500

    New Comments11

    hbmpoleTz

    MY BROTHER DAMU YANGU

    Tanzania

    shaa baby 7sf44

    nampend xn nedy

    Tanzania

    joeboymusic

    ngoma kali

    Tanzania

    140887497

    nakukubali broo

    Tanzania

    chrisa de xtopper

    nakubali

    Tanzania

    EUGEN MOLLEL03pgr

    hakika

    Tanzania

    Jizzo Monster

    unyamaa mwingi Sana

    Tanzania

    mrsinia

    nedy mkali sana

    Tanzania

    mrsinia

    Namkubar sana nedy music hasa kwa wimbo wake wa "Only you" yaan ni bonge 1 la song kwang

    Tanzania

    Kidoboyrkyq1

    Good historical background

    Tanzania

    Jofrey chid

    vpee

    Tanzania

    +

        -   or   -

        -   or   -

        NG +234

            Please Select A Playlist

            Add New Playlist

            Share on

            Embed: Love & Light EP

            Custom Size :

            • Default
            • Desktop(300*600)
            • Mobile(300*250)

            Type :

            • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
            Get Boomplay Premium
            for
            Payment Method
            Pay With
              Review and pay
              Order Date
              Payment Method
              Due Today
              Flutterwave
                Subscription Successful

                Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

                Now you have access to all the features of Boomplay App.
                Payment Failed

                Please check your balance and then try again.

                You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
                Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
                Payment Processing...
                10 s

                Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

                Payment Processing
                Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
                About Order Status