Boom Top | Ngoma 10 kali kati ya 100 ambazo zimefanya vizuri Boomplay wiki hii
Leo ni Jumatatu murua, siku ambayo tunamulika ngoma ambazo zimefanya vizuri ndani ya orodha ya ngoma 100 wiki iliyopita.
Katika kuhakikisha hili linakwenda vizuri, tunakusogezea ngoma 10 ambazo zimeongoza kwenye chati wiki iliyopita.
1. Nitongoze ft. Diamond Platnumz - Rayvanny
Ni ngoma kutoka kwa staa wa muziki Tanzania, Rayvanny 'Nitongoze'. Ngoma hii mpaka sasa imeendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kukaa nafasi ya kwanza katika orodha ya ngoma 100 bora Boomplay.
Nitongoze ft. Diamond Platnumz
2. Yataniua ft. Diamond Platnumz - Mbosso
Yataniua ni ngoma ambayo inapatikana kwenye EP mpya ya Mbosso inayojulikana kwa jina la Khan. Ngoma hii yenye mahadhi ya Amapiano ni kali sana na amemshirikisha Diamond Platnumz. Endelea kusikiliza ngoma hii hapo chini.
3. Nidhibiti ft. Zuchu - Jux
Huu ni wimbo kutoka kwenye albamu ya Jux 'King Of Hearts'. Ni ngoma kali ambayo imepambwa kwa ustadi wa juu na uwepo wa msanii mahiri wa muziki Tanzania, Zuchu.
4. Huyu Hapa
'Huyu Hapa' pia ni ngoma kutoka kwa Mbosso inayopatikana kwenye EP yake ya 'Khan'. Ni ngoma ya kwanza kabisa kwenye EP na ina ladha fulani ya miondoko ya mduara. Inapendeza sana kupigwa kwenye sherehe hususani harusi.
5. Kwikwi - Zuchu
Ngoma hii kutoka kwa Zuchu Kwikwi ni ya Mapenzi ambayo Zuchu anaonesha ni kwa kiasi gani anampenda mpenzi wake huku akimsihi mpenzi wake huyo asimuache kwani anaogopa kuumbuka na kupata aibu mbele za watu.
6. Champion ft. Nay Wa Mitego - Kontawa
Ngoma hii kali kutoka kwa Kontawa ni kali na inazidi kudhihirisha ubora wake kadri siku zinavyozidi kwenda. 'Champion' ni ngoma fulani ya kutia moyo inayoelezea mapambano ya maisha. Uwepo wa Nay Wa Mitego umezidi kuongeza chachu ya wimbo huu kuwa bora zaidi. Sikiliza ngoma hii hapo chini.
7. Shetani ft. Costa Titch & Alfa Kat
Ngoma hii ya Amapiano kutoka kwa Mbosso akiwashirikisha Costa Titch & Alfa Kat inapatikana kwenye albamu yake ya 'Khan'. Ni bonge moja la ngoma ambayo haichoshi kusikiliza muda wote.
Shetani ft. Costa Titch & Alfa Kat
8. Cough (Odo) ft. Empire - Kizz Daniel
Baada ya kutamba muda mrefu na ngoma yake Buga (Lo Lo Lo), ngoma nyingine ya Kizz Daniel 'Cough (Odo)' imeanza kutamba kwa kuingia kumi kumi bora ya 100 bora ndani ya app ya Boomplay.
9. Nakupenda - Jay Melody
Ni ngoma kali kutoka kwa Jay Melody huku ikiwa ni miongoni mwa ngoma zinazochezwa sana kwa sasa kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki. Imeendelea kufanya vizuri na kwa sasa imeshika nafasi ya sita kutoka nafasi ya tano wiki iliyopita.
10. Rush - Ayra Starr
Kwa mara ya kwanza, ngoma hii iliingia kumi bora wiki tatu zilizopita. Ni ngoma kali kutoka kwa Ayra Starr ambayo haichoshi kusikiliza. Endelea kusikiliza hapo chini.
Wimbo gani umekuvutia kwenye orodha hii?
#BuzzBrandColumn #BoomTop #Music #Trending
Comments (11)
New Comments(11)
Juma Hamisuy04h
MBÃJĪ BØYÏ
dah yani ni unyam mwingi
chickselt3j
kwa kwl i can see
Eric_ msimbaziguvumoja
hii risti me kiukweri sijaipenda kabisa
pia unaweza kusikiliza nyimbo hii kama wewe haupo single ${href0}
moschinoqf0py
good
Kephas Jacksonbw9y7
Great
Thonnykiss
Duu! Kiukwel mnanikosha nangoma zenu
stephenaugustino@
that nice..
144478794
nice
Daudi Msangi
kabisa
TanzaniaBoomone1
pia unaweza kusikiliza nyimbo hii kama wewe haupo single ${href0}
no ten ngoma kali sanaaaa