Boom Fresh | Ngoma kali zilizoachiwa wiki hii na zinapatikana Boomplay hizi hapa
Leo ni Ijumaa ya murua kabisa, siku ambayo huwa tunakusogezea ngoma ambazo zimeachia wiki nzima kwaajili ya kukukumbusha kusikiliza ngoma hizo endapo utakuwa umepitwa kutokana na shughuli mbalimbali za kila siku.
Wiki hii tumeshuhudia wasanii wakiachia ngoma mbalimbali. Wasanii hao ni Harmonize (Weed Language ft Konshens), Platform (Nileweshe), G Nako (Hiyo Hapo), Man Fongo (Binadamu), Country Wizzy (One Call Away), Beka Flavour (Kua Uone), Jay Melody (Acha Wivu), Aslay (Follow Me ft Harmonize), Nacha (Simuachi)
Nileweshe - Platform
Msanii wa muziki anayekuja kwa kasi kubwa, Platform ameachia wimbo wake mpya 'Nileweshe'. Ni ngoma mpya ya mapenzi ambayo ni nzuri kuisikiliza. Bofya hapa kuisikiliza kwa urefu wake.
Hiyo Hapo - G-Nako
Staa wa muziki Tanzania, G-Nako amekuja na ngoma yake mpya 'Hiyo Hapo'. Ngoma hii kali inaendelea kufanya vizuri kwenye chati za muziki na bado inatikisa hadi sasa. Hata video ya wimbo huu ameitendea haki sana. Endelea kusikiliza ngoma hii hapo chini.
Binadamu - Man Fongo
Staa wa muziki wa Singeli, Man Fongo amedondosha mkwaju mpya 'Binadamu'. Ni ngoma kali ambayo inazungumzia jinsi binadamu walivyo na hulka tofauti. Sikiliza ngoma hii hapo chini kupitia Boomplay.
One Call Away - Country Wizzy
Mkali wa muziki wa trap, Country Wizzy ameachia ngoma yake mpya inayofahamika kwa jina la 'One Call Away'. Sikiliza ngoma hii hapo chini kupitia Boomplay.
Kua One - Beka Flavour
Beka Flavour amerudi tena kwa mara nyingine na kuachia wimbo wake mpya ambao ameupa jina la 'Kua Uone' akimshirikisha EASY MAN. Sikiliza ngoma hii hapo chini kupitia Boomplay.
Acha Wivu - Jay Melody
Mkali wa muziki nchini Tanzania, Jay Melody amekuja tena na ngoma mpya ya Amapiano 'Acha Wivu'. Ni ngoma yake ya kwanza kabisa ya miondoko ya Amapiano. 'Acha Wivu' inakuja baada ya kupita miezi kadhaa kufuatia ngoma yake ya 'Nakupenda' kufanya vizuri sana kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki. Sikiliza mkwaju huu mpya 'Acha Wivu' kutoka kwa Jay Melody hapo chini.
Follow Me ft Harmonize - Aslay
Baada ya kimya kirefu, hatimaye staa wa Bongo Fleva, Aslay amekuja na ujio mpya na kuachia ngoma mpya 'Follow' Me. Ni ngoma ya kwanza kwa mwaka huu tangu alivyoachia ngoma yake ya mwisho mwaka 2021. Umepokeaje ujio mpya wa Aslay?
Simuachi - Nacha
Rapa kutoka Tanzania, Nacha ameachia ngoma yake mpya 'Simuachi' ambayo amemshirikisha Mattan. Sikiliza ngoma hii hapo chini.
Ngoma gani umeikubali zaidi kati ya hizi zote?
#BuzzBrandColumn #BoomFresh #Music #Trending
Comments (14)
New Comments(14)
#eliudiyiug
131401316
Aslay follow me
david davis gpv9
Cooooooool
oss95yr4
boomplay mmetisha saaaana wanetu...
Godfrey Paulotcgu1
good song
LIONEL TEMMI
good song
Tatu82ar5
zuchu
davy machumbe
boom
Frank de fighter
,[0x1f630]
nuel FAM
perfect
iddy ht5of
[0x1f633][0x1f633]
Fida Paul248
g00d s0ng
waoo