Boom Focus | Tunamuangazia Harmonize
Kwenye Boom Focus, leo hii tunamuangazia staa wa muziki nchini Tanzania ambaye ni bosi wa Konde Music Worldwide, Harmonize.
Ni msanii ambaye kwa sasa, wanapotajwa wasanii watano wakubwa Afrika Mashariki hawezi kukosa kwenye orodha.
Historia yake kwenye muziki ipo wazi na watu wengi wanaofuatilia muziki watakuwa wanafahamu hilo. Alianzia kwenye lebo ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz na baadaye kujiengua kusimama kama msanii anayejitegemea.
Baada ya kujenga misingi imara, Harmonize aliamua kuanzisha lebo yake ambayo ameipa jina la Konde Music Worldwide na ina jumla ya wasanii ambao ni Ibraah, Anjella, Killy, Cheed, Skales and Harmonize mwenyewe.
Kutokana na umahiri wa ngoma zake, Harmonize amefanikiwa kufanya kolabo na wasanii mbalimbali barani Afrika kama vile Burna Boy, Morgan Heritage, Khaligraph Jones, Yemi Alade na wengine wengi.
Ameachia ngoma nyingi ambazo zimefanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali kama vile Kwangwaru, Bedroom, Jeshi, Bakhresa, Attitude na nyingine nyingi.
Pamoja na ngoma nyingine nyingi, Harmonize amefanikiwa kuachia albamu mbili ambazo ni Afro East na High School, huku pia akiwa na EP moja ambayo ni Afro Bongo.
Kwa sasa anatamba na EP yake ya 'Made For Us'. Sikiliza 'Made For Us' EP kutoka kwa Harmonize hapo chini kupitia Boomplay;
#BuzzBrandColumn #BoomFocus #Music #Harmonize #MadeForUs
Comments (6)
New Comments(6)
001 barayandema
official contawa
ana pamban kwa ajili ya mziki ufike mbali
nikjina anajituma san
official contawa
nikjina anajituma san
BALOGE TV
Big up sana kaka hamo
BALOGE TV
.
yuko vizuri sana