Boom Milestone | Albamu ya Jux 'King Of Hearts' yafikisha zaidi ya streams mil 1 Boomplay
Albamu ya staa wa muziki wa R&B, Jux 'King Of Hearts' imefanikiwa kufikisha zaidi ya streams milioni 1 kwenye app ya Boomplay.
Idadi hii ya streams imekuja ikiwa zimepita takribani siku tatu tangu kuachiwa kwa albamu hii. 'King Of Hearts' iliachiwa Novemba 25, 2022.
Albamu hii ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wote wa muziki kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla.
Kwa muda mrefu, Jux alikuwa akidokeza ujio wa albamu hiyo kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano mbalimbali ambayo alikuwa akifanya na mpaka kufikia hatua ya kuachia orodha ya nyimbo za albamu hiyo ya 'King Of Hearts'.
Katika albamu hiyo, imeshuhudiwa Jux akifanya kolabo na wasanii mahiri ndani na nje ya Tanzania kama vile wa Bien kutoka Kenya, Patoranking wa Nigeria, Mbosso wa WCB, Marioo, Zuchu katika ngoma ya 'Nidhibiti' na wakali wengine wengi wa muziki.
Ngoma zilizomo kwenye albamu hii ni 'Lucky Now', 'Sina Neno', 'Sing For You', 'I Love You', 'Mapepe', 'My Mind', 'Simuachi', 'Nidhibithi', 'Kitanda', 'Only You I See', 'Found Love', 'Number One', 'Wena', 'Show Dem', 'Sumu' na 'Nice (Kiss)'.
Vile vile 'Kings Of Hearts' inahusisha watayarishaji mahari wa muziki kama vile S2kizzy, Bob Manecky, Foxx Made It, Kapipo, Tony Duardo, Abbah Process na wengine.
Hii ni albamu ya pili kutoka kwa Jux. Albamu yake ya kwanza inafahamika kwa jina la 'The Love Album' na ilimpa sifa na kuimarisha jina lake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa sasa, 'King Of Hearts' imefanikiwa kufikisha streams milioni 1.3. Endelea kusikiliza albamu hii mahiri kutoka kwa Jux.
#BuzzBrandColumn #BoomMilestone #Music #Trending #Jux #KingOfHearts
Comments (1)
New Comments(1)
BerryNipeys
Cv