Loading...

Download

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Leo ni Ijumaa ya murua kabisa, siku ambayo huwa tunakusogezea ngoma ambazo zimeachia wiki nzima kwaajili ya kukukumbusha kusikiliza ngoma hizo endapo utakuwa umepitwa kutokana na shughuli mbalimbali za kila siku.


Wiki hii tumeshuhudia wasanii wakiachia ngoma mbalimbali, EP pamoja na albamu. Wasanii hao ni Rayvanny (Unplugged Session EP), Jux (King Of Hearts), Rosa Ree (My Cherie), Meja Kunta (Demu Wangu), Kassim Mganga (Hapa Kati), Mr Blue (Baby Boo), Moni Centrozone (Toto), Kusah (Te Amor), Chin Bees (Ball Remix), Rosa Ree (Goddess), Marioo (My Life),


Unplugged Session - Rayvanny

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Rayvanny ameshusha tena kifurushi kipya baada ya kuachia EP yake ya 'Unplugged Session'. Hii inakuwa EP ya nne kwa Rayvanny tangu aanze rasmi kutambulika kwenye muziki. EP nyingine ni 'Vanny Boy', 'Flowers' na 'Flowers II'.


'Unplugged Session EP' ina jumla ya ngoma 8 ambazo ni 'Mzuri', 'I Love You', 'Mtoto', 'Nateswa', 'Mwamba', 'Mama', 'Vacation' pamoja na 'Nipigie'. Kwenye 'Unplugged Session EP', Rayvanny amemshirikisha msanii mmoja pekee ambaye ni Fari by Dar Kid.

Unplugged Session

King Of Hearts - Jux

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Baada ya subira ya muda mrefu, hatimaye staa wa muziki wa R&B nchini Tanzania, Jux ameachia albamu ya 'King Of Hearts' ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.


Katika albamu hiyo yenye jumla ya ngoma 16, imeshuhudiwa Jux akifanya kolabo na wasanii mahiri ndani na nje ya Tanzania kama vile wa Bien kutoka Kenya, Patoranking wa Nigeria, Mbosso wa WCB, Marioo, Zuchu katika ngoma ya 'Nidhibiti' na wakali wengine wengi wa muziki.

King of Hearts

My Cherie - Rosa Ree

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Rapa mahiri wa kike, Rosa Ree amekuja na ngoma nyingine mpya ambayo inafahamika kwa jina la 'My Cherie'. Hii ni neno linalotokana na lugha ya Kifaransa ambalo linamaanisha 'Mpenzi wangu'. Sikiliza ngoma hii kwa urefu zaidi hapo chini kupitia Boomplay.

My Cherrie

Demu Wangu - Meja Kunta

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Msanii mahiri wa Singeli, Meja Kunta ameachia wimbo mpya ambao ameupa jina la 'Demu Wangu' akiwashirikisha Mabantu. Kama ilivyo kawaida, Meja Kunta huwa hakosei na hakika kwenye ngoma hii amewapa mashabiki wake kile alichozoea kuwapa, huku uwepo wa Mabantu ukiongeza ladha nyingine.

Demu Wangu ft. Mabantu

Hapa Kati - Kassim Mganga ft. AY Masta

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Gwiji wa muziki wa kubembeleza kutoka Tanga, Kassim Mganga amewakumbuka mashabiki wake baada ya kuachia ngoma mpya ambayo ameipa jina la 'Hapa Kati' akimshirikisha gwiji mwingine wa muziki Tanzania, AY Masta. Una maoni gani kuhusu ngoma hii?

Hapa Kati ft. Ay Masta

Baby Boo - Mr Blue

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Gwiji wa muziki wa Bongo Fleva, Mr Blue ameachia ngoma mpya ambayo ameipa jina la 'Baby Boo' akiwashirikisha Ibraah & Baddest 47. Ni ngoma kali yenye flow matata ambayo unaweza kuisikiliza Boomplay pekee. Bofya hapo chini kusikiliza 'Baby Boo' kutoka kwa Mr Blue.

Baby Boo ft. Ibraah & Baddest 47

Toto ft. Country Wizzy - Moni Centrozone

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Moni Centrozone ameachia dude jipya akimshirikisha Country Wizzy. Ngoma inafahamika kwa jina la 'Toto'. Sikiliza kwa urefu ngoma hii hapo chini kupitia Boomplay.

Toto ft. Country Wizzy

Te Amor - Kusah

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Kusah ameachia mkwaju mpya 'Te Amor'. Ni ngoma kali ambayo imezidi kuwa tamu zaidi kwa umahiri wa sauti yenye mvuto kutoka kwa Kusah. Isikilize ngoma hii hapo chini.

Te Amor

Ball Remix Chin Bees

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Mkali wa trap, Chin Bees ameachia dude jipya 'Ball Remix'. Sikiliza kwa undani hapo chini kupitia Boomplay.

Ball (Remix) ft. William Last KRM

Goddess - Rosa Ree

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Mwanadada Rosa Ree amekuja na albamu yake mpya yenye ngoma kali sana ambayo ameipa jina la 'Goddess'. Goddess maana yake ni Mwanamke mahiri. Albamu hii ina jumla ya ngoma 17. Bofya hapo chini kusikiliza albamu nzima.

Goddess

My Life - Marioo

Boom Fresh | Ngoma zote zilizoachiwa wiki hii hizi hapa, ngoma gani kali zaidi?

Siku chache baada ya kufikisha streams milioni 100 Boomplay, Marioo ameachia mkwaju mwingine matata akiupa jina la 'My Life'. Ni ngoma ambayo inazungumzia maisha yake na maisha kwa ujumla. Sikiliza ngoma hii hapo chini kupitia Boomplay.

My Life

Ngoma gani imekuvutia zaidi kati ya zote zilizoachiwa wiki hii?

#BuzzBrandColumn #BoomFresh #Music

Comments (32)

0/500

    New Comments32

    122398496

    @0682478216

    Tanzania

    122398496

    vvvp

    Tanzania

    jeremiah shamter

    hbbp,p,p0,,

    Tanzania

    tougeousr@gmail.com

    Hi

    Tanzania

    Ronex Kayela

    [0x1f60e][0x1f60e]

    Tanzania

    Chree Jacky

    [0x1f605]

    Tanzania

    ELIA JB

    social media Jobs https://eliamwapinga.aweb.page/p/fb08a7e9-2479-47db-9c77-6633d9c7b36a

    Tanzania

    aminamwela7@gmail.com

    mabatu kaua

    Tanzania

    Vannie Curl

    nice[0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f]

    Tanzania

    Memphiso7tja

    Ameizng

    Tanzania

    husna shem

    good

    Tanzania

    neyllanvd82i

    very nice♥️♥️♥️

    Tanzania

    +

        -   or   -

        -   or   -

        NG +234

            Please Select A Playlist

            Add New Playlist

            Share on

            Embed: Love & Light EP

            Custom Size :

            • Default
            • Desktop(300*600)
            • Mobile(300*250)

            Type :

            • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
            Get Boomplay Premium
            for
            Payment Method
            Pay With
              Review and pay
              Order Date
              Payment Method
              Due Today
              Flutterwave
                Subscription Successful

                Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

                Now you have access to all the features of Boomplay App.
                Payment Failed

                Please check your balance and then try again.

                You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
                Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
                Payment Processing...
                10 s

                Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

                Payment Processing
                Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
                About Order Status