Boom Fresh | Hizi ni ngoma mpya ambazo zimeachiwa wiki hii na zinapatikana Boomplay
Leo ni Ijumaa ya murua kabisa, siku ambayo huwa tunakusogezea ngoma ambazo zimeachia wiki nzima kwaajili ya kukukumbusha kusikiliza ngoma hizo endapo utakuwa umepitwa kutokana na shughuli mbalimbali za kila siku.
Wiki hii tumeshuhudia wasanii wakiachia ngoma mbalimbali. Wasanii hao ni Kontawa (Champion Remix ft. Harmonize), Timbulo (Tamu), AY Masta (Waves), Jux (Wena), Tunda Man (Sema), K2GA (Nifundishe), Hamadai (Masusu).
Champion Remix ft. Harmonize - Kontawa
Baada ya ngoma yake Champion ft Nay Wa Mitego kufanya vizuri, Kontawa amerudi tena na kufanya remix ya Champion akimshirikisha Harmonize. Ni bonge moja la ngoma ambayo inazungumzia zaidi mapambano ya maisha huku uwepo wa sauti ya Harmonize ukiongeza vionjo zaidi na kupendezesha ngoma hii.
Tamu - Timbulo
Mkali wa kitambo kwenye game ya Bongo Fleva amewaonjesha mashabiki wake ladha nzuri ya muziki wake ambao wameikosa kwa muda mrefu kwa kuachia ngoma mpya 'Tamu'. Ngoma hii inapatikana Boomplay kwa kubofya hapo chini
Waves - AY Masta
Gwiji wa Bongo Fleva na Hip Hop, AY Masta ameachia mkwaju wake mpya unaofahamika kwa jina la Waves. Ni ngoma yake ya pili kwa mwaka huu wa 2022 na kama vile ndiyo ngoma yake ya kufungia mwaka. Sikiliza 'Waves' kutoka kwa AY Masta hapo chini kupitia Boomplay.
Wena ft. Khanyisa & Yumbs - Jux
Mkali wa miondoko ya R&B, Jux amewashibisha mashabiki wake na ngoma mpya 'Wena'. Hii ni ngoma yake ya sita kwa mwaka huu. Sikiliza 'Wena' hapo chini.
Sema ft Kontawa - Tunda Man
Tunda Man ameendelea kuwapa burudani mashabiki wake kwa kuachia ngoma mpya 'Sema' ikiwa imepita miezi michache tangu alipoachia EP yake ya 2022. Ni ngoma kali kama ambavyo imekuwa kawaida ya Tunda Man.
Nifundishe - K2GA
Staa huyu kutoka kwa Kings Music ameachia mkwaju wake mpya ambao ameupa jina la 'Nifundishe'. Ni ngoma yake ya pili kwa mwaka huu wa 2022 ikitanguliwa na 'Rangi Rangi'. Bofya hapo chini kusikiliza ngoma hii hapo chini.
Mususu - Hamadai
Msanii wa Bongo Fleva mwenye sauti ya aina yake, Hamadai ameamua kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuachia ngoma mpya 'Mususu'. Sikiliza ngoma hii hapo chini.
#BuzzBrandColumn #BoomFresh #Music
Comments (3)
New Comments(3)
BerryNipeys
Gman Kajad Official
listen my new release ${href0}
Gman Kajad Official
great jams
Cool