Boom Milestone | EP ya Mbosso 'Khan' yafikisha streams milioni 10 Boomplay
Siku kadhaa zimepita tangu mwanamuziki kutoka lebo ya WCB, Mbosso achangamstasnia ya muziki Tanzania baada ya kuachia EP yake mpya ya 'Khan', tayari EP hiyo imefanikiwa kufikisha streams milioni 10 kwenye app ya Boomplay.
'Khan' ni EP ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na hata namna ilivyozinduliwa ilithibitisha namna Mbosso na uongozi mzima wa WCB ulivyokusudia kukata kiu ya wapenzi wote wa muziki wa Tanzania na nje ya mipaka.
Uzuri wa EP hii ni kwamba imechanganya mahadhi na vionjo mbalimbali ya muziki kama vile muziki wa mduara, Bongo Fleva pamoja na Amapiano, huku kukiwa na mchanganyiko wa lugha za Kiswahili, Kispaniola na kiarabu.
'Khan EP' imeshirikisha wasanii kadhaa wakubwa kutoka ndani na nje ya Afrika kama vile bosi wake Diamond Platnumz, mwanadada Ruby, Mohamed Almanji, Costa Titch pamoja na Alfa Kat. Hii ni EP ya kwanza kabisa kutoka kwa Mbosso tangu aanze kujishughulisha rasmi na muziki.
'Khan EP' imejumuisha ngoma 6 za moto ambazo zimebeba maudhui ya mapenzi kwa kiasi kikubwa. Ngoma zilizopo kwenye EP hii ni 'Huyu Hapa', 'Pole', 'Shetani', 'Wayo', 'Assalaam' pamoja na 'Yataniua'. Wasanii ambao wameshirikishwa kwenye EP hii ni Ruby, Costa Titch, Ya Levis, Mohammed Almanji na Diamond Platnumz.
Kwa uchache, huu ni uchambuzi mfupi kwa baadhi ya ngoma zilizopo kwenye albamu hii:
Huyu Hapa
Hii ni ngoma ya kwanza kwenye EP hii. Imeundwa na vionjo vya muziki wa mduara kwa kiasi fulani vikichanganyika na Bongo Fleva. Ndani ya ngoma hii, Mbosso anaeleza ni kwa namna gani amezama kwenye penzi zito na mpenzi wake.
Pole ft. Ruby
Ni ngoma kali ambayo imechagizwa na sauti nzuri na kuvutia kutoka kwa mwanadada mahiri Ruby. Kwenye ngoma hii Ruby na Mbosso wanatoa pole kwa watu wasiopenda penzi lao kuendelea kumea. Huu ni muendelezo wa ngoma za mapenzi kwa Mbosso ambazo hakika ni jadi yake.
Shetani ft. Costa Titch & Alfa Kat
Alichofanya Mbosso kwenye ngoma hii ni kwamba ameleta utofauti kwa kutengeneza Amapiano ambayo ina mdundo mkali lakini pia ina mashahiri makali yanayovutia na yanayoeleweka. Ngoma hii imetengenezwa na S2kizzy.
Kusikiliza EP nzima ya 'Khan' kutoka kwa Mbosso kupitia Boomplay, bofya hapo chini.
#BuzzBrandColumn #BoomMilestone #Music #Trending #Mbosso
Comments (44)
New Comments(44)
rejina offical
anneryot28
nyimbo tamu kweriiii
alikabu
[0x1f630][0x1f630][0x1f630][0x1f630]
Kamu Mwangaby9ku
nimependa sana
150893749
hajakaa sawa
Ditto Pileee649
namkubal kinoma
150868868
mboso
Daud Mtui
ni kelele ingine
Neema Mafiewoold
atar sana nimeipenda [0x1f641][0x1f641]
Ÿøûńg Åśâp fęrk
g g g g g g g g g g t g g t t t t t t t t t t t t t y y y y t g y y t y t y y y y g y y y y y y y y y y y y y y y y y
yusuphv3tke
yusuphv3tke
hatamimi nimeiyelewa kinoma moma
i likes your songs mbosso[0x1f618][0x1f618]