Boom Focus | Tunamzungumzia Nay Wa Mitego
Nay Wa mitego ni moja wa wasanii wanaokubalika sana hapa Tanzania kutokana ana aina ya muziki aliochagua kufanya.
Kwa walioanza kumfuatilia rapa huyu, tangu anaanza kujulikana kwa nyimbo kama Itafamika, wanaelewa kuwa muziki anaofanya Nay ndiyo wa hivyo siku zote. Ni rapa ambaye ameamua kucgahua kuzungumza mada ngumu ambazo ni mara chache sana kuzungumzwa na wengine.
Hupendelea zaidi kuzungumza ukweli unaakisi uhalisia wa maisha ya jamii husika na mara nyingi huchoma, na ndiyo sababu inawawia vigumu marapa wengine kufanya anachofanya.
Hulka yake hii ndiyo ilimfanya kuanza kujilikana na watu kwa haraka zaidi tangu alivyoanza kusikika mwaka 2009 kupitia ngoma yake ya 'Itafahamika'.
Amekuwa akitoa ngoma za kurekebisha, kukosoa, kuelimisha na kuburudisha pia. Amepita milima na mabonde mengi lakini bado ameendelea kusimama imara na kuwapa mashabiki wake kile wanapenda kusikia kutoka kwake.
Miongoni mwa ngoma zake ambazo zimewahi kutamba sana ni 'Hello', 'Salamu Zao', 'Muziki Gani', 'Nasema Nao', 'Mapenzi Au Pesa', 'Pale Kati Patamu', 'Amsha Popo', 'Kaa Mbali Nao', 'Mwaka Wa Roho Mbaya' na ngoma nyingine kali nyingi.
Septemba mwaka huu aliachia albamu yake kali ambayo ameipa jina la 'Rais Wa Kitaa' yenye jumla ya ngoma 14.
Ngoma yake anayotamba nayo kwa sasa ni 'Sauti Ya Watu' ambayo anazungumza mambo mbalimbali ya kijamii. Endelea kusikiliza 'Sauti Ya Watu' hapo chini kupitia Boomplay.
#BuzzBrandColumn #BoomFocus #Music #NayWaMitego
Comments (19)
New Comments(19)
djohodotv 6hdy0
obed6g1wu
pga kaz
Melania Donalt
jamani mungu fundi
saimoni Aloyce
anajua sahna mwamba namkubari sahna acha atusemee wanyonge make xie hatuezi sema chchte hikali haito kuja kujirudia won love nay
Paulo Temba
sauti ya watu
alfred hoya5zw5j
mzalendo,wa kweri baba yaga
Gilbert Santos
Sauti ya kitaaa
jofreykisinda21@gmail.com
nay mtu mkubwa
nasibu naziru9tqiy
anatisha mwamba nauho ndo uzalendoo
Reubenm6344
Bogus nyie
Amos Madenge 24
mwamba uyuapa
aureliaalh27
yupo good namkubali sana asa katika ngoma yake ya salamu zao
***