Boom Fresh | Hizi ndizo nyimbo zilizoachiwa wiki hii na zinapatikana Boomplay
Leo ni Ijumaa ya murua kabisa, siku ambayo huwa tunakusogezea ngoma ambazo zimeachia wiki nzima kwaajili ya kukukumbusha kusikiliza ngoma hizo endapo utakuwa umepitwa kutokana na shughuli mbalimbali za kila siku.
Wiki hii tumeshuhudia wasanii wakiachia ngoma mbalimbali. Wasanii hao ni , Mbosso (Khan) na Harmonize (Made For Us), Menina (Changuta), Mansuli (Love Life Album), Salmin Swaggz (Flight Mode Album), G Nako (Tusipangiane), Kontawa (Champion), Ommy Dimpoz (Anaconda).
Mbosso - Khan EP
Staa wa muziki kutoka WCB Wasafi, Mbosso rasmi ameachia EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ambayo ameipa jina la 'Khan'. 'Khan' ni EP ya kwanza kabisa kutoka kwa Mbosso tangu aanze kujishughulisha rasmi na muziki.
'Khan' ni EP kali ambayo imejumuisha ngoma 6 za moto ambazo zimebeba maudhui ya mapenzi kwa kiasi kikubwa. Ngoma hizo ni 'Huyu Hapa', 'Pole', 'Shetani', 'Wayo', 'Assalaam' pamoja na 'Yataniua'. Wasanii ambao wameshirikishwa kwenye EP hii ni Ruby, Costa Titch, Ya Levis, Mohammed Almanji na Diamond Platnumz.
Harmonize - Made For Us
Staa wa muziki nchini Tanzania na bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize ameachia albamu yake mpya ambayo ameipa jina la 'Made For Us'. Hii ni albamu ya tatu ya Harmonize tangu aanze kufanya muziki rasmi. Albamu hii inakuja takribani mwaka mmoja kupita baada ya albamu yake ya pili 'High School' ambayo aliiachia Novemba 5, 2021.
'Made For Us' ni albamu yenye jumla ya ngoma 14, huku baadhi ya ngoma hizo zikiwa tayari zilikwishaachiwa mapema kabisa kabla ya albamu hii kuachiwa. Ngoma hizo ni 'Amelowa', 'Nitaubeba', 'Deka', 'Miss Bantu', na 'Leave Me Alone'.
Menina - Changuta
Mwanadada Menina amekuja na ngoma mpya ambayo ameipa jina la 'Changuta'. Menina ameachia ngoma hii ikiwa umepita muda mfupi sana baada ya ngoma yake nyingine ya 'Tabia Zangu' Sikiliza hapo chini ngoma hii mpya ya Menina 'Changuta'.
Mansuli - Love Life
Rapa Mansuli ameamsha mji baada ya kuja na albamu yake mpya matata yenye ngoma 20 za moto. Albamu hii yote inapatikana Boomplay na unaweza kusikiliza hapo chini.
Salmin Swaggz - Flight Mode
Salmin Swaggz amedondosha project mpya matata 'Flight Mode' Albamu hii ina jumla ya ngoma 17 na ni project ya kwanza kabisa kutoka kwake kwa mwaka huu wa 2022. Sikiliza albamu nzima ya Salmin Swaggz 'Flight Mode' hapo chini kupitia Boomplay.
G Nako - Tusipangiane
Mkongwe katika game ya muziki Tanzania, G Nako amekuja na mkwaju wake mpya 'Tusipangiane'. Hii ni project ya pili kwa G Nako kwa mwaka huu wa 2022. Endelea kusikiliza ngoma 'Tusipangiane' hapo chini kupitia Boomplay.
Ommy Dimpoz - Anaconda
Ommy Dimpoz, moja ya wasanii wenye sauti mahiri sana ameachia ngoma yake mpya 'Anaconda'. Ngoma hii ni kama kidokezo kuelekea ujio wa albamu yake mpya ambayo muda wowote kutoka sasa inaweza kuachiwa.
#BuzzBrandColumn #BoomFresh #Trending #Music
Comments (35)
New Comments(35)
99599383
mariakinabo7@gmail.com
nice songs[0x1f618]
Ally Dushu
Good song
KIRONDO BOY
Good
Dickson Ndaro
nice
nevy*mash
mwendo wa kurefresh[0x1f609] vya arusha tutavilaje
kado 4 life1zkhy
good
dayo1reg5
i really love boomplay
Deborah 716ed
chirisipha myagila
Mwanahamis Jumahyvmb
nice
enock switibatijws7x
ongera
Aisha omary8tmua
nice
Nyimbo mpya