New Music | Mbosso aachia EP yake mpya 'Khan', ngoma ya ipi umeikubali?
Staa wa muziki kutoka WCB Wasafi, Mbosso rasmi ameachia EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ambayo ameipa jina la 'Khan'.
'Khan' ni EP ya kwanza kabisa kutoka kwa Mbosso tangu aanze kujishughulisha rasmi na muziki.
'Khan' ni EP kali ambayo imejumuisha ngoma 6 za moto ambazo zimebeba maudhui ya mapenzi kwa kiasi kikubwa.
Ngoma hizo ni 'Huyu Hapa', 'Pole', 'Shetani', 'Wayo', 'Assalaam' pamoja na 'Yataniua'. Wasanii ambao wameshirikishwa kwenye EP hii ni Ruby, Costa Titch, Ya Levis, Mohammed Almanji na Diamond Platnumz.
Uzuri wa EP hii ni kwamba imechanganya mahadhi mbalimbali ya muziki kama vile muziki wa mduara, Bongo Fleva pamoja na Amapiano, huku kukiwa na mchanganyiko wa lugha za Kiswahili, Kispaniola na kiarabu.
Kusikiliza EP nzima ya 'Khan' kutoka kwa Mbosso kupitia Boomplay, bofya hapo chini.
#Trending #Music #Khan #Mbosso #KhanEP
Comments (5)
New Comments(5)
zachemistry
minnah7b2ju
zote wallah[0x1f647]
mamushkacom37
Good
joente fleva Tz
ipopowa kan
Digital BenLee
unyamaaa ni mwingi sanaa
yataniua ft diamond platnumz