Loading...

Download

Boomplay na CAPASSO zaendeleza makubaliano ya kimkakati, kuneemesha watunzi na waimbaji muziki

Boomplay na CAPASSO zaendeleza makubaliano ya kimkakati, kuneemesha watunzi na waimbaji muziki

App na jukwaa linaloongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki, Boomplay limeingia makubaliano ya ushirikiano na Chama kinachosimamia hakimiliki za watunzi na waimbaji wa muziki (CAPASSO) ikiwa ni mkakati wa Boomplay kuendelea kupanua huduma zake barani Afrika.


Mpango huo unaifanya CAPASSO kuwa na mamlaka ya kukusanya na kusimamia mirabaha ya uchapishaji kwa niaba ya wasanii na watunzi wa maudhui mbalimbali ya muziki kutoka nchi tano hadi ishirini katika bara la Afrika.


Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi wa Maudhui na Mikakati wa Boomplay, Phil Choi amesema kuwa, leseni hiyo ya makubaliano inaendeleza maono na dhamira ya Kampuni kuuwezesha muziki wa kiafrika kuwa na uwezo, thamani na hadhi kubwa.


Phil alisema: “Tangu kuanza kwa ushirikiano wetu mwaka 2015, CAPASSO imekuwa mmoja wa washirika wetu wa karibu katika kuhakikisha watunzi barani Afrika wanapata sehemu ya haki yao ya mirabaha kupitia kazi zao. Shauku yetu kubwa ni kuhakikisha tunawajibika katika kuchangia kwa ukuaji mkubwa wa tasnia ya muziki barani Afrika kupitia ushirikiano wa kimkakati kama huu.


"Ushirikiano huu utaendelea kusaidia uwepo wa mfumo wa kuaminika wa kiikolojia kwa wasanii na wachapishaji, na tunaweza kutarajia kutengeneza njia zaidi za mapato kwa wasanii kupitia mtandao wa washirika wetu."


Jotam Matariro ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CAPASSO, ameunga mkono hoja za Choi, na kusema kuwa, "Lengo kuu la CAPASSO ni kuhakikisha kwamba watunzi wa nyimbo wa Kiafrika na wachapishaji wao wanapata thamani ya haki ya kazi zao. Hivyo ni fursa muhimu kushirikiana na wadau kama Boomplay, ambao mara kwa mara huwekeza katika mnyororo kamili wa thamani wa tasnia ya muziki wa Kiafrika. Ni kupitia utaratibu huo ndipo sekta nzima inaweza kuendelea kukua.”


Boomplay, ambayo inajivunia zaidi ya watumiaji milioni 60 kwa mwezi ikiwa na katalogi kubwa ya muziki yenye nyimbo zaidi ya milioni 60, ina shirikiana na lebo zote kubwa za ndani na nje ya Afrika na wasambazaji wa kazi za muziki. kuu zote na lebo na wasambazaji bora wa Kiafrika na Kimataifa.


Jukwaa hili hivi karibuni lilitangaza kuingiza takwimu za wasanii wa Afrika katika chati maarufu Duniani za Billboard.


Aidha, mafanikio haya na mengine mengi yamechangia kuimarisha nafasi zao katika kilele cha soko la upakuaji na usikilizaji muziki la Afrika.

Comments (3)

0/500

    New Comments3

    £Ã~Yonna_Tz

    Safi

    Tanzania

    128426625

    arikiba

    Tanzania

    Fidelis Welwel

    Safi

    Tanzania

    +

        -   or   -

        -   or   -

        NG +234

            Please Select A Playlist

            Add New Playlist

            Share on

            Embed: Love & Light EP

            Custom Size :

            • Default
            • Desktop(300*600)
            • Mobile(300*250)

            Type :

            • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
            Get Boomplay Premium
            for
            Payment Method
            Pay With
              Review and pay
              Order Date
              Payment Method
              Due Today
              Flutterwave
                Subscription Successful

                Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

                Now you have access to all the features of Boomplay App.
                Payment Failed

                Please check your balance and then try again.

                You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
                Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
                Payment Processing...
                10 s

                Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

                Payment Processing
                Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
                About Order Status