Loading...

Download

#BoomplayAwards: Mbosso abeba Tuzo nane Boomplay

'BoomplayAwards: Mbosso abeba Tuzo nane Boomplay

Staa wa muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi, Mbwana Yusuph Kilungi 'Mbosso' amefanikiwa kukabidhiwa tuzo (plaques) nane kutoka Boomplay baada ya nyimbo zake kufanya vizuri kwenye app ya Boomplay.


Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Mbosso kupata tuzo kutoka Boomplay. Mwaka jana Mbosso alipata tuzo tatu kupitia nyimbo zake za 'Nadekezwa', 'Hodari' pamoja na 'Tamu'.


Mwaka huu Mbosso amefanya kufuru ya Tuzo baada ya kupata tuzo nane ikiwa ni ongezeko ya tuzo tano kutoka zile tatu za mwaka jana.


Mwaka huu amepata tuzo kupitia ngoma zake za 'Fall', 'Tamu', 'Nadekezwa', 'Haijakaa Sawa', 'Tamba', 'Maajab', 'Hodari' (nyimbo zote hizi zimepata streams milioni moja kila moja) pamoja na tuzo ya jumla baada ya kufikisha jumla ya streams milioni 20.

'BoomplayAwards: Mbosso abeba Tuzo nane Boomplay

Haya ni mafanikio makubwa sana kwa Mbosso, kwani amekuwa miongoni mwa wasanii wachache ambao wamepata tuzo nyingi mwaka huu.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiz, Mbosso ametoa shukrani kwa mashabiki wake maana wao ndiyo wamefanya afike alipo sasa na bila wao yeye si chochote.


"Namshukuru Mungu, nawashukuru pia mashabiki wangu kwa kuendelea kuwa karibu na mimi, ku-stream kazi zangu, ku-download na waendelee kusapoti. Zawadi ni za kwetu wote.


Mbosso amesema siri ya mafanikio ya kupata tuzo hizo hana yeye isipokuwa mashabiki wake kwa sababu wao ndio wanaosikiliza kazi zake.

'BoomplayAwards: Mbosso abeba Tuzo nane Boomplay

Amewaasa wasanii wenzake ambao bado hawajaamua kutumia fursa za platform kama Boomplay kutangaza kazi zao zaidi basi wafanye hivyo kwani kwa sasa dunia ndiyo imehamia huko.


"Kwa wasanii wenzangu ambao bado wako nyuma, basi ni wakati wao kutumia vizuri platforms hizi kwa sababu zinatusaidia kutangaza muziki wetu lakini pia tunapata hela," amesema Mbosso.


Mbosso amesema ngoma zilizompatia tuzo hizo anaziheshimu sana kwa sababu ndio zilizomtambulisha kwa kiasi kikubwa na kujulikana kwa mashabiki wengi wa muziki.


Kwa sasa Mbosso anatamba na albamu yake ya Definition Of Love, sikiliza hapo chini;

Definition Of Love

#Trending #Music #BoomplayAwards #Mbosso

Comments (103)

0/500

    New Comments103

    azizahgb8qv

    nakukubal

    Tanzania

    azizahgb8qv

    vzr

    Tanzania

    103857606

    [0x1f618]

    Tanzania

    sechelela davd

    [0x1f618]

    Tanzania

    yuzoedxa9

    nice artist.

    Tanzania

    elly ellydld51

    congrats

    Tanzania

    Juma Salumuclqt3

    nc

    Tanzania

    121899322

    congratulations my brother, may God bless you.

    Tanzania

    124045710

    nyimbo mpya

    Tanzania

    10377091

    massive

    Ghana

    Alvind30mu

    Epic

    Kenya

    ONABULE ABIODUN KOLADE

    cool

    Nigeria

    +

        -   or   -

        -   or   -

        NG +234

            Please Select A Playlist

            Add New Playlist

            Share on

            Embed: Love & Light EP

            Custom Size :

            • Default
            • Desktop(300*600)
            • Mobile(300*250)

            Type :

            • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
            Get Boomplay Premium
            for
            Payment Method
            Pay With
              Review and pay
              Order Date
              Payment Method
              Due Today
              Flutterwave
                Subscription Successful

                Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

                Now you have access to all the features of Boomplay App.
                Payment Failed

                Please check your balance and then try again.

                You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
                Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
                Payment Processing...
                10 s

                Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

                Payment Processing
                Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
                About Order Status