Loading...

Download
  • Genre:Gospel
  • Year of Release:2022

Lyrics

SURRENDER - AMBWENE MWASONGWE

...

Yesu, na "sarenda" mambo yangu kwako

Maana wewe u mwaminifu

Kweli naogopa kukabidhi haya

Nimekuja tuzungumze

Ulikuwa shujaa nilipokuwa vitani

Nilipoumwa njaa ulikuwa mkate

Nilipohitaji sadaka kwa fidia ya dhambi

Ulifanyika kondoo nikashinda kwa Nguvu

Uliwakemea waliponinyamazisha

Ukawazuia waliponidhibiti

Ukaonyesha njia katika ya hila

Ukategua fumbo nikashinda kwa Nguvu

~

Nakushauri mjue Sana Mungu wako

Ili uwe na Amani moyoni

Ndivyo hayo mema yatakujia

Ninaogopa usipofanya hivyo moyo

Utapoteza utulivu wa ndani

Utahangaika na kuumia

Utapata taabu Sana wee moyo

Ukiwa bize kuchunguza watu na vitu

:::::::::::-:::::::::::::

Nimefanya kosa kuhesabu vya mwilini

Na kujidhania maskini

Kumbe nina utajiri wa rohoni

Unaozidi vya mwilini

Wewe umenipa vitu pesa haiwezi nunua

Umegawa bure vya thamani visivyo na bei

Pumzi, usingizi, hamu ya kula

Na afya

Kitanda, chakula na dawa visingeweza kunipa

Nitanunua bunduki

Sitanunua uhai

Nitanunua zawadi

Ila sio kupendwa

Nitanunua dawa

Ila sio uzima

Nitanunua mapambo

Ila sio uzuri

::::::::-:::::::::

Sitayaogopa yatishayo wanadamu

Wayaonayo ni makubwa

Ninakuamini Mungu wangu

Uwezaye kumeza kimezacho tembo

Wewe huyawazi yale yanipayo mawazo

Unawaza mema yaletayo Amani, Tumaini

Katikati ya magumu kana kwamba napoteza

Hata katika hayo nauona Wema wako

Wewe hutangazi yale sisi Twatangaza Sana

Twatangaza jambo mwanzo pale likishatokea

Wewe unatangaza mwisho wa jambo tangu mwanzo

Nitaficha ujinga wangu

Kukumbuka kukaa kimya

~

Nakushauri(moyo) mjue Sana Mungu(sikiliza) wako

Ili uwe na Amani moyoni (kama unatakaka)

Ndivyo hayo mema yatakujia (utulivu)

Ninaogopa(moyo) usipofanya hivyo

Moyo utapoteza utulivu wa ndani

Utahangaika na kuumia

Utapata taabu Sana wee moyo

Ukiwa bize kuchunguza watu na vitu

Nakushauri mjue Sana Mungu wako

Ili uwe na Amani moyoni

Ndivyo hayo mema yatakujia

Ninaogopa usipofanya hivyo

Moyo utapoteza utulivu wa ndani

Utahangaika na kuumia

Utapata taabu Sana wee moyo

Ukiwa bize kuchunguza watu na vitu

:::

Utapata taabu Sana wee moyo

Ukiwa bize

Kuchunguza

Watu na vitu

*

Similar Songs

+

      -   or   -

      -   or   -

      NG +234

          Please Select A Playlist

          Add New Playlist

          Share on

          Embed: Love & Light EP

          Custom Size :

          • Default
          • Desktop(300*600)
          • Mobile(300*250)

          Type :

          • HTML/HTML5 (WordPress Supported)
          Get Boomplay Premium
          for
          Payment Method
          Pay With
            Review and pay
            Order Date
            Payment Method
            Due Today
            Flutterwave
              Subscription Successful

              Congratulations! You have successfully activated Boomplay 1 Month Premium.

              Now you have access to all the features of Boomplay App.
              Payment Failed

              Please check your balance and then try again.

              You'll lose your subscription if we don't have a working payment method for your account, so please check your payment details.
              Need help? Contact Boomplay Subscription Support.
              Payment Processing...
              10 s

              Payment is being processed by . Please wait while the order is being comfirmed.

              Payment Processing
              Your order is processing, and it may take up to a few days for the service provider to handle your payment. Please kindly stay tuned and check your order status in ‘User Center’.
              About Order Status